Tunayo story kutokea kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma ambapo amesema Majaji wa zamani walikuwa hawapendi kurudi darasani wala kusoma.
Profesa Juma ameyasema hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akizungumza na Majaji wapya 15 walioteuliwa hivi karibuni, ambapo amesema majaji hao lazima wapate elimu endelevu.
Amesema kuwa Mahakama ya Tanzania imekuwa na utaratibu mara baada ya kupata Majaji ama watumishi wapya kuwapa kuna kuwa na mpango wa elimu endelevu na kuwakaribisha mahakamani ili wajue mambo ya msingi watakayokumbana nayo.
“Lazima wafahamu changamoto zinazowakabili, kwani majaji wa zamani walikuwa hawapendi kurudishwa darasani na kusoma, hivyo dunia ya sasa mambo yanabadilika sana,”amesema.