Wanawake duniani kote wanaungana leo Ijumaa Machi 8 kusherehekea siku ya kimataifa ya Wanawake, wakitafakari yale ambayo wamefikia kufikia sasa ambapo kwa ngazi ya Mkoa yatafanyika katika Uwanja wa Mji Mwema-Kigamboni Dar es Salaam
Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ambayo pia inajulikana kama IWD, ilianzia katika harakati za wafanyakazi na ikawa tukio la kila mwaka linalotambuliwa na Umoja wa Mataifa.
Siku hii ilianza mwaka wa 1908, wakati wanawake 15,000 waliandamana katika jiji la New York wakidai muda mfupi wa kazi, mishahara bora na haki ya kupiga kura. Kwa zaidi ya karne moja, dunia nzima imefanya Machi 8 kuwa siku maalumu kwa wanawake.
Siku hii iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1911, huko Austria, Denmark, Ujerumani na Uswisi. Miaka 100 iliadhimishwa mwaka 2011, hivyo mwaka huu tunaadhimisha Kitaalamu Siku ya 112 ya Kimataifa ya Wanawake.
Siku ya Kimataifa ya Wanawake imekuwa siku ya kusherehekea jinsi wanawake walivyofikia katika jamii, siasa na uchumi, huku mizizi ya siku hiyo ikimaanisha migomo na maandamano yanafanywa ili kuongeza uelewa juu ya ukosefu wa usawa unaoendelea.