Maafisa 16 wa Uhifadhi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii , Idara ya Wanyamapori Makao Makuu Dodoma, NCAA, TANAPA, TAWA na Mweka -CAWM wanahudhuria Warsha ya Mafunzo ya Uhifadhi Wanyamapori (Seminar in wildlife conservation ) nchini China, katika Chuo Cha National Academy of Forestry and Grassland Administration kuanzia tarehe 16 -29 Oktoba 2023.
Masuala yatakayofundishwa ni pamoja na jinsi China ilivyofanya mapinduzi ya kiuchumi kupitia Sera nzuri za uhifadhi na matumizi endelevu ya Maliasili kupitia Chama Tawala Cha Chinese Communist Party (CPC) na watu wake, jinsi ya kuhifadhi Wanyamapori adimu na ambao wako hatarini kutoweka, kuifanya china kuwa ya kijani ili kupunguza hewa ukaa na kufuta umaskini ambao lengo limefikiwa mwaka 2021.
Na kushirikiana na mataifa mbalimbali ⁷katika kutekeleza mikataba ya Kimataifa, kuendeleza Utalii wa Wanyamapori na maeneo ya kihistoria, kutumia kilimo hususan misitu kama chanzo kikuu cha ajira vijijini, kutunza vyanzo vya maji na kadhalika.