Katika tukio la kutisha, Maafisa wawili wa Jeshi walio mafunzoni walishambuliwa kikatili pamoja na marafiki zao wa kike katika Wilaya ya Indore, Madhya Pradesh, siku ya Jumanne huko India.
Shambulio hilo lilitokea karibu na Jam Gate ambapo kundi lenye silaha liliwashambulia kwa lengo la kuwapora.
Kundi hilo la Wanaume wanane waliokuwa na bastola, visu, na magongo lilivamia kundi hilo la Maafisa, likiwapiga Maafisa na wanawake kabla ya kuwanyang’anya fedha na mali zao, kisha baadaye, walimchukua mmoja wa Maafisa na Mwanamke mateka, huku wakiwatuma Maafisa wengine kwenda kuchukua fedha za fidia ya rupia milioni 10.
Afisa aliyesalia alirudi haraka katika kitengo chake na kutoa taarifa kwa Kamanda wake, ambaye aliwaarifu Polisi, Polisi na WanaJeshi walienda eneo la tukio, lakini Washambuliaji walikimbia walipoona magari yakikaribia, Tukio hilo lilitokea ndani ya eneo la kituo cha polisi cha Badgonda.
Aidha Maafisa hao walikuwa na umri wa miaka 23 na 24, na walikua wakifanya mafunzo ya Young Officers katika Shule ya Infantry huko Mhow.
Baada ya tukio hilo Maafisa hao wamepelekwa Hospitalini kwa uchunguzi wa kimatibabu na Madaktari walithibitisha majeraha yao na kubaini kuwa mmoja wa Wanawake alibakwa, Kesi ya uhalifu huo tayari imesajiliwa na msako wa kuwakamata washukiwa unaendelea.