Mkuu wa mkoa wa Iringa , Halima Dendego kwa niaba ya Rais Dkt . Samia Suluhu Hassan ametoa misaada mbalimbali kwa kaya 140 katika kata ya Mboliboli tarafa ya Pawaga halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikiwemo vitu mbalimbali kama vile chakula na dawa kwenye kaya zilizo athiriwa na maafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha zaidi ya siku tatu katika eneo hilo na kusababisha kifo cha mtu mmoja .
Akizungumza na wanannchi hao Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego ametoa pole kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amewataka wanannchi kuzidi kuchukua tahadhari ya mvua hizo ambapo mamlaka imeripoti kwamba kutakuwa na mvua nyingi
Pia Dendego amesema baada ya maafa hayo kutokea kama serikali wameendelea kuzidi kuboresha miundombinu iliyoharibiwa na mvua kubwa kama madaraja na barabara ambapo miundombinu hiyo iliharibika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kupelekea maji kuzidi kwenye madaraja na kukosa muelekeo na kuelekea kwenye makazi ya watu .
Vilevile Rc Dendego alifika kutoa pole nyumbani kwa familia kwa mwanaume aliyepoteza maisha kutokana na maafuriko hayo .
Baada ya mvua hizo kubwa kunyesha Takriban kaya 140 ziliachwa bila makazi na bila chakula na mtu mmoja kupoteza maisha na huku zikisababaisha uharibifu wa mashamba , miundombinu ya barabara, umeme na maji katika vijiji vinavyopatikana katika tarafa hiyo .