Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani humo, kuharakisha uchunguzi wa tukio la mauaji ya Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya wa Shirika la Wamisionari wa Afrika Michael Samson (63), Raia wa Nchi ya Malawi ili wahusika wachukuliwe hatua.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema upelelezi umeanza na wanaendelea kupata viashiria mbalimbali vinavyodaiwa kuhusika kwenye tukio hilo.