Wafanyabiashara na wenye viwanda wameshauriwa kushiriki katika mafunzo yanayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania TBS ili kuweza kupata uelewa zaidi kuhusu masuala yanayohusu viwango.
Akizungumza katika ofisi za TBS Jijini DSM, Mkuu wa kitengo cha Mafunzo TBS, Prisca Kisella amesema mafunzo ni muhimu kwani yanasaidia wadau kufikia vigezo vya viwango,taratibu za uthibiti ubora wa bidhaa na mifumo, pamoja na kukidhi matakwa ya kanuni na sheria zinazohisiana na biashara yake pia kumpunguzia mteja ule urasimu pindi anapokuwa anahitaji huduma za TBS.
“Mafunzo haya yanajikita zaidi katika kutoa uelewa kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo, viwango na matumizi ya viwango vya Tanzania (National Standards) katika uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali” Prisca
“Matumizi ya viwango vya kimataifa katika mifumo ya usimamizi wa kimenejimenti (ISO standards), taratibu za kuthibitisha ubora wa bidhaa, taratibu za kuthibitisha mifumo ya usimamizi ya kimenejimenti katika maeneo ya uzalishaji na huduma” Prisca
“Taratibu za kupeleka bidhaa nje (Technical Asssistance for export – TAE) pamoja na taratibu za kuingiza bidhaa nchini hususani kwenye kukidhi matakwa ya viwango na ubora” Prisca
“NAENDA KUMWAMBIA MUNGU KILA KITU” MANENO YA MTOTO MDOGO KABLA HAJAFARIKI KWA MABOMU