Ni Belti Masala akisimulia tukio la kushangaza lililomkuta mdogo wake anayeitwa Albert Masala mwenye umri wa miaka 32 ambaye inadaiwa alitekwa na watu wasiojulikana nyumbani kwao eneo la Kagoma lililopo Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ambapo inadaiwa walichukua hela kisha wakaacha wamemtundika msalabani kama Yesu na kumtelekeza porini karibu na kanisa ambapo aliokolewa na wasamalia wema na anaendelea vizuri mimi ni Lameck Richard na hii ni report kutokea Muleba Mkoani Kagera.