Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye ni mgombea wa urais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameweka wazi kuwa mkutano wao visiwani Zanzibar si wakufanya kampeni bali ni kwa ajili ya kuwashukuru Wazanzibar.
“Kwanza kabla sijasema lolote naomba kuweka wazi, tumekusanyika hapa si kwa mkutano wa kampeni ,kampeni bado tunajua kwa upande wa Zanzibar kampe zinaanza tarehe Septemba 11 tunakuwa na siku 45 za kufanya kampeni” Maalim Seif
“Naomba niwashukuruni nyote ambao tangu alfajiri mmesubiri wagombea kwa hamu kubwa hata chai hamkunywa, lakini kwa sababu ya mapenzi ya kweli kwa chama chetu na wagombea wetu mmekubali mbaki ilimuwasalimu na kuwakaribisha hapa Zanzibar” Maalim Seif
TAZAMA WALICHOFANYA WAPENZI WA ACT WAZALENDO ZANZIBAR