Siku 6 zimepita kulikuwa na taarifa za Wachimbaji wakionesha kumkataa Muwekezaji mgodi wa Bulumbaka uliyopo Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu, May 05 2021, Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya amefika eneo la mgodi wa Bulumbaka lenye mgogoro kuongea na Wachimbaji kisha kutoa maamuzi ya Wizara, kabla ya kutoa maelekezo ya Serikali Naibu Waziri alitoa nafasi ya kuwasikiliza Wachimbaji pamoja na Kaimu Afisa Madini ambae ni miongoni mwa waliolalamikiwa na Wachimbaji.