Waziri Mkuu wa zamani wa Ivory Coast Pascal Affi N’Guessan Jumamosi aliteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Popular Ivorian Front (FPI) katika uchaguzi wa rais wa 2025.
Katika kongamano huko Yamoussoukro, mji mkuu wa Ivory Coast, N’Guessan alichaguliwa tena kuwa rais wa FPI kwa 99.34% ya kura zilizopigwa na baadhi ya wapiga kura 4,500.
FPI ni chama cha Rais wa zamani Laurent Gbagbo. N’Guessan alichukua uongozi wake wakati wa kufungwa kwa Gbagbo huko The Hague kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
N’Guessan amewania urais mwaka wa 2015 na 2020, kila mara akishindwa na Alassane Ouattara, aliyemaliza muda wake.
Alikataa matokeo na alikamatwa kwa muda mfupi kwa tuhuma za kuendesha ‘serikali sambamba’.
Baadhi ya mapendekezo muhimu ya N’Guessan ni pamoja na kufuta seneti na kurejeshwa kwa ukomo wa mihula ya urais.
Ouattara ambaye alishinda uchaguzi tena kwa njia ya kutatanisha hajasema iwapo atawania muhula wa nne.