Nchini Senegali, zaidi ya wiki moja baada ya uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa rais kutoka Februari 25 hadi Desemba 15, 2024, mzozo kati ya mamlaka na wapinzani kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi unaendelea.
Wakati maandamano makubwa yalipangwa na mashirika ya kiraia kufanyika Februari 12 huko Dakar, gavana wa mji mkuu alipiga marufuku maandamano hayo, na kushinikiza waandaaji kuahirisha maandamano haya dhidi ya kuahirishwa kwa kura kwa dakika za mwisho na rais kuongezwa muhula.
Nchini Senegal, hadi usiku wa manane, waandaaji, karibu na mashirika hamsini ya kiraia, wanasema walijaribu kupata makubaliano kutoka kwa gavana kuhusu barabara watakazotumia kwa maandamano hayo; bila mafanikio.
Siku ya Jumanne asubuhi tena, mmoja wa wanachama wa jukwaa hili walitazamowa kukitana na Halmashauri ya wilaya ili kujaribu kuhalalisha barabara waandamanaji watakatumia kwa maandamano yao.
Tarehe mpya na ratiba mpya inatarajia kupendekezwa wakati wa mchana. “Tunataka kubaki katika sheria na kuepuka vurugu zozote,