Naibu Katibu Mkuu Bara CHADEMA, Benson Kigaila amesema maandamano waliyopanga kufanyika January 24,2024 yapo kama kawaida na wamekubaliana na Jeshi la Polisi mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi na usalama.
Akizungumza na Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam amesema;
“Tumepeleka barua, tumeeleza njia za kupita na ajenda yetu kwa mujibu wa sheria bahati nzuri jana Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam alitupigia simu akatupa wito wa kukutana nao leo saa Tano asubuhi, niwape tu taarifa tumekutana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam pamoja na timu yake yote kuanzia saa Tano asubuhi hadi saa Tisa Alasiri tumejadiliana vyakutosha kuhusu mambo kadhaa ikiwemo root tutazopita na usalama utakuaje,”.
tazama pia….