Kiongozi wa upinzani Nchini Uganda, Dkt. Kizza Besigye amekamatwa na amefunguliwa mashtaka ya uhalifu baada ya kuitisha maandamano ya kupinga kupanda kwa bei za bidhaa muhimu na kutaka Serikali kuingilia kati na kudhibithi ongezeko hilo.
Besigye, alikamatwa Mei 24 katika Kituo cha Polisi cha Nagalama hiyo ni baada ya kuwatoroka akari waliokuwa wakilinda nyumbani wake akitakiwa kutotoka nyumbani hapo kwa muda wa wiki tatu.
Alisema: “Ni lazima Serikali ya Rais Yoweri Museveni ihakikishe inatoa ushuru kwa bidhaa muhimu ili kuwezesha raia kuzinunua kwa bei nafuu.”
Mwendesha Mashtaka wa Serikali amesema Mahakamani kuwa alichofanya Besigye kuitisha maandamano inalenga kusababisha uharibifu wa mali.