Watu 21 wameuawa katika maandamano nchini Msumbiji, tangu mahakama ya juu ilipoidhinisha ushindi wa chama cha Frelimo siku ya Jumatatu.
Idadi hiyo ya vifo imetolewa na wizara ya mambo ya ndani.
Maandamano makubwa yamekuwa yakiendelea Msumbiji tangu mahakama ya katiba ilipoidhinisha ushindi wa Frelimo, makundi ya upinzani na wafuasi wao wamesema uchaguzi ulikuwa na udanganyifu.
Watu 78 wamekamatwa kufikia sasa na usalama umeimarishwa kote nchini.
Waziri wa mambo ya ndani Pascoal Ronda ameliambia shirika la utangazaji la serikali TVM kwamba jeshi la serikali limeimarisha usalama katika mji mkuu Maputo na katika sehemu muhimu za nchi.
Chama cha Frelimo kimekataa madai ya wizi wa kura.