Msanii kutokea kiwanda cha muziki Tanzania, Country Wizzy ameachia ngoma yake mpya inayoitwa Current Situation akiwa amemshirikisha nyota kutokea Rockstar Africa Young Lunya.
Current Situation ni ngoma ya tano kutoka kwa Country Wizzy kwa mwaka huu wa 2023 akiwa tayari ameachia ngoma nyingine kama One Call Away, Oright, Shake Dat Ass, Let It Go na Ooouh
Daz Naledge ndiye amehusika katika kuandaa ngoma hii kama producer huku video ya ngoma hii ikiwa inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.
Kwa sasa Country Wizzy yuko chini ya label ya Bxtra Records , zamani ikiwa inajulikana kama B Hits.
Kando na Country Wizzy, Bxtra Records pia inasimamia wasanii wengine wawili ambao ni fundi wa Amapiano Jaivah pamoja na Meja Kunta.