Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga April 8, ametembelea Bandari ya Kibirizi iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kuongea na wamiliki wa boti zinazofanya safari zake Kigoma kwenda Burundi na DR Congo huku akisisitiza suala karantini ni lazima.
Akiongea na wamiliki hao amesema “kwa sasa lazima kwa mabaharia wanaosafiri kwenda Nchi jirani kwa lengo la biashara kama Congo na Burundi huko mnaporejea tutawaweka maeneo maalumu yaliyotengwa kwa lengo la kupima afya zenu”
“Baada ya siku kumi na nne mtarudi kufanya shughuli zenu kama afya yako itaonekana kuwa vizuri, kwa wale wanaotoka karantini tumeandaa utaratibu wa kuwapa vyeti ili kumtambulisha huko mnapokwenda”.
“WAZAZI WANACHOKA WATOTO, WANAULIZA MSALABA UTAISHA LINI” MWANASAIKOLOJIA