Leo April 8, 2016, Mahakama kuu kanda ya Mwanza imetangaza maamuzi ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge iliyofunguliwa na Ezekiel Wenje tangu 25.11.2015, aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana kutaka Mahakama kupitia upya mchakato wa kujumlisha Matokeo ya Uchaguzi Mkuu October 2015 kati yake na Mbunge wa sasa Stanslaus Mabula, Shauri hilo lililokuwa linasikilizwa na Jaji Kakusuro Sambo kwenye Mahakama Kuu kanda ya Mwanza.
Maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ni kwamba wajibu maombi hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mleta Shauri hana ushahidi wa kuithibitishia Mahakama kwamba matokeo yaliyotangwazwa sio halali, millardayo.com imezipata picha za tukio zima.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE