Askofu Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (CAG), Mtume Dk. Dunstan Maboya amewataka Watanzania wafanye kazi kwani njaa ni mbaya ndio maana inasababisha uwepo wa ‘Machawa’.
Mtume Maboya ameyasema hayo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa ametoka nje ya Nchi ambapo ametumia neno Chawa akiwa na maana ya watu wanaopenda kuwa wapambe ili wajipatie Pesa.
“Njaa ni mbaya, njaa inaweza kusababisha wambeya wanakuwa wengi hapa Mjini mtu anapeleka news za uongo uongo tu anakuwa Chawa ili alishwe, sasa vitu kama hivyo sio vizuri na utakuta wengi wanaokuwa Machawa hawana kitu kwa sababu ni wavivu na uvivu ni dhambi”
“Ningependa Watanzania tusiwe wavivu kuna vitu vitatu muhimu lazima upate kibali mbele ya Mungu, Serikali na mbele za wazazi,” amesema Mtume Maboya.
Akizungumzia ziara yake Nje ya Nchi ikiwe katika nchi ya Sudan amesema “Mfano katika nchi ya Sudan utakuta Mungu amewabariki wana mashamba mengi sana na mto Nile ni mkubwa mno lakini wameshindwa kulima kwa sababu ya vita, hivyo tuombe Mungu vita visitokee katika nchi yetu”
Kwa upande wake Pastor Christina Mbelwa wa Kanisa la Valley of Life amesema “Kama nchi nyingine zimeona mazuri aliyonayo na akaenda kuwafundisha ina maana na sisi kwetu tunatakiwa tufunguke macho tuweze kuwatumia watu hao ambao Mungu ametupatia kwenye nchi yetu wataweza kutuelekeza kutufundisha na kutusaidia kutoka hatua moja kwenda nyingine,”.