Mahakama ya kikatiba nchini Madagascar, imeunga mkono ushindi wa rais Andry Rajoelina katika uchaguzi wa urais wa tarehe 16 mwezi Novemba.
Upinzani ulikuwa umesema uchaguzi huo haukufanyika kwa uhuru na haki na kulikuwepo na udaganyifu, madai ambayo mahakama imetuipilia mbali.
Kwa mujibu mahakama, rais Rajoelina alipata asilimia 59 ya kura katika uchaguzi ambao asilimia 46 ya wapiga kura walishiriki.
Idadi kubwa ya wanasiasa wa upinzani walikataa kushiriki zoezi hilo ambapo wamesisitiza kuwa hawatambui matokeo ya uchaguzi huo.
Rajoelina mwenye umri wa miaka 49, aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka wa 2009 baada ya mapinduzi yalioangusha utawala wa rais wa zamani Marc Ravalomanana.
Rajoelina, meya wa zamani wa mji mkuu wa Antananarivo, anatuhumiwa na wapinzani wake kwa kushiriki ufisadi, kuingiwa na tamaa pamoja na kufumbia macho changamoto zinazowakabili raia.