Wito umetolewa kwa wananchi kujitokeza kupima Afya zao katika kambi ya madaktari Bingwa kutoka Taasis ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa .
Wito huo umetolewa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt.Scholastica Malangalila wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kambi itakayokaa kwa siku tano kuanzia tarehe 15-19/04/2024 katika hospitali hiyo.
Amesema lengo la kambi hiyo ni kusogeza huduma kwa wananchi kupitia Wizara ya Afya ambayo imewezeshwa na Serikali inayoongozwa na Mh.Rais Samia Suluhu Hassan ili kuwapunguzia gharama wananchi kufata huduma hizo JKCI
Dkt.Malangalila amesema wanatarajia kuhudumia zaidi ya wagonjwa 800 katika siku tano za kambi hiyo kwasababu katika siku ya kwanza mpaka saa nne asubuhi tayari walikuwa wameshaandikisha wagonjwa 120.
Naye Dkt.Pedro Palangyo Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo kutoka Taasis ya Moyo ya Jakaya Kikwete amesema kumekuwa na changamoto ya ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza kutokana na aina ya Maisha Kama unywaji wa pombe kupita kiasi,uvutaji wa sugars,ulaji usiofaa,matumizi ya chumvi na Sukari,kutokufanya mazoezi pamoja na unene uliopitiliza.