Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo tarehe 23 Juni, 2016 imekabidhi taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa taarifa hiyo, Rais Magufuli amesema kwa sasa uchaguzi umekwisha na ametaka watanzania wote wajielekeze kufanya kazi na kwamba serikali yake haitavumilia vitendo vyovyote vitakavyoathiri utekelezaji wa ahadi zake kwa watanzania katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.
>>>’Yapo tuliyoyaahidi kuyatekeleza kwa wananchi katika kipindi cha miaka mitano, nisingependa kuona mtu yeyote ananichelewesha kuyatekeleza hayo niliyoyaahidi, nasema nisingependa kuona mtu yeyote ananichelewesha kuyatekeleza hayo niliyoyaahidi katika kipindi cha miaka mitano’
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KAELEZA SABABU YA KUSIMAMISHA AJIRA MPYA KWA MUDA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE