Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imesema kuna changamoto ya upungufu wa fedha za uendeshaji na za Utekelezaji wa miradi ya uwekezaji ambayo inachochea ukuaji wa Sekta ya Utalii kwakuwa bajeti iliyokuwa inatumika kwa Hifadhi 16 ndio hiyohiyo inayotumika sasa kwa Hifadhi 22, pamoja na kanda nne, vituo 5 vya Malikale na Ofisi 2 Kiunganishi zilizopo Dar es Salaam na Dodoma.
Akiwasilisha taarifa hiyo Bungeni jijini Dodoma leo February 7, 2023 Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa amaesema hali ya upungufu wa fedha inapelekea Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kushindwa kuitika kwa haraka kwenye shughuli za dharura, ulinzi na usalama na kuzorota kwa utoaji wa huduma za kitalii kwa kuwa uwekezaji unaofanywa kwenye hifadhi hizi haufanywi kwa ufanisi, hivyo kupelekea kukosa tija iliyokusudiwa.