MKUU wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Judith Nguli amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kutoa elimu kwa wananchi ili kufahamu umuhimu wa uwekezaji unaotaka kufanywa na kampuni ya DP World.
Dc Nguli ameyasema hayo wakati akitoa salama za Wilaya kwenye kikao cha Madiwani ambapo amesema kumekua na wimbi la watu wakipotosha kuhusu uwekezaji huo jambo ambalo limekua na mkanganyiko wa wananchi.
Anasema Rais Samia Suluhu Hassani anafanya kazi kubwa ya kuwaletea Maendeleo wananchi hivyo ni lazima wajue umuhimu wa mkataba huo ambao unafanywa na Serikali ili waendelee kuiamini Serikali yao.
Dc Nguli ameongeza kwa kusema endapo wapotoshaji wataendelea kuzungumza na wananchi wakawasikiliza watakua na upendo mdogo kwa nchi yao hivyo madiwani wananafasi kubwa ya kutoa elimu hiyo.
Aidha Dc Nguli ameitaka kamati ya nidhamu kumchukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa Idara ya Kilimo,mifugo na uvuvi halmshauri hiyo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka .
Dc Nguli anasema mkuu huyo wa Idara amekua akiwanyanyasa watumishi wenzake wa idara hiyo jambo ambapo linarudisha nyuma utendaji kazi wao hivyo pamoja na kua tuhuma hizo zipo kwenye uchunguzi lakini kamati hiyo inatakiwa itende haki kwa kumwajibisha mkuu huyo wa idara endapo atakuwa na makosa hayo.
Nao Madiwani hao wamesema kwa sasa watafanya mikutano kwenye kata zao ili kuzungumza na wananchi kuhusu umuhimu wa mkataba wa uwekezaji wa bandari Kupitia Kampuni ya DP World
Madiwani hao wanasema Rais Samia amekua akitoa fedha nyingi za maendeleo kwenye kata zao hivyo jukumu lao ni kuzungumzia mema yote anayofanya kwa maslai ya Taifa kwani hawezi kuuza bandari kama watu wanavyodai.