VODACOM Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara ya magwiji waliocheza kwa mafanikio makubwa katika klabu ya Real Madrid.
Kikosi cha magwiji hao maarufu kama `Real Madrid Legends` kitafanya ziara ya siku nne nchini kuanzia Agosti 22 mwaka huu na kitacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya kikosi maalumu cha nyota wa Tanzania.
Meneja wa ziara hiyo Dennis Ssebo amesema ziara hiyo ni mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya mkurugenzi wake mkuu, Farough Baghozah na meneja wa ziara hiyo ni Dennis Ssebo.
Wachezaji wa Real Madrid waliocheza La Liga miaka ya nyuma, ligi ya mabingwa kombe la dunia kama vile Mfaransa Zinedine Zidane, Mreno Luis Madeila Figo na Mbrazil Ronaldo de Lima watakuwepo katika ziara hiyo.
Ssebo kabla ya mkutano wa leo, aliiambia millardayo.com kuwa maandalizi ya ziara hiyo yanakwenda vizuri na itakuwa fursa pekee kwa Watanzania kuiona Real Madrid kwa mara ya kwanza barani Afrika.
“Ninaloweza Kusema ni kwamba, Watanzania wakae tayari kupokea wachezaji 27 wa zamani wa timu ya Real Madrid na mashabiki 23 kutoka Hispania wanaokuja kuwashangilia magwiji wao, kwa hiyo kwa jumla tunapokea watu 50 kutoka Hispania kwa ajili ya ziara hii”
“Ni ziara ambayo tulifikiria itakuwa fupi lakini wenzetu kumbe wameipenda nchi na wanaifahamu, kwahiyo ni ziara ambayo itachukua takribani siku nne”
Ungana na mimi kwenye twitter instagram na facebook niwe nakutumia kila kinachonifikia iwe usiku au mchana mtu wangu, bonyeza hapa >>> INSTA TWITTER FB
Source:Shaffihdauda.com