Msimu mpya wa soka nchini Hispania umefunguliwa rasmi jana usiku kwa mchezo wa Spanish Super Cup kati ya mabingwa wa Copa Del Rey Real Madrid dhidi ya mabingwa wa La Liga Atletico Madrid.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu, uliisha kwa matokeo ya sare ya 1-1.
Kiungo mshambuliaji wa Colombia aliyesajiliwa Madrid hivi karibuni, James Rodriguez alifunga goli lake la kwanza katika klabu hiyo kwenye dakika ya 81 ya mchezo huo, kabla ya Raul Garcia kuisawazishia Atletico dakika 7 baaadae na kuiwezesha timu yake kupata sare kwenye mchezo huo wa kwanza wa Spanish Super Cup.
Kwenye mchezo huo, mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo alishindwa kumaliza mechi hiyo kutokana na kupata maumivu ya mgongo yaliyompelekea kumpisha James Rodriguez dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza.
Unaweza kuangalia magoli ya mechi hiyo hapa chini