Takriban waandamanaji 70,000 siku ya jumapili waliandamana mjini Prague kulalamikia mfumuko wa bei ikiwemo ongezeko la bili za nishati na kutaka kusitishwa kwa vikwazo dhidi ya Urusi kutokana na vita vya Ukraine na kuitaka serikali ya sasa kujiuzulu.
Viongozi wa mrengo wa kulia na wa mrengo mkali wa kushoto waliungana katika mkutano wa Jamhuri ya Czech kutaka makubaliano mapya na Moscow kuhusu usambazaji wa gesi na kusitishwa kwa utumaji silaha kwa Ukraine, huku wakiitaka serikali ya mrengo wa kulia ya waziri mkuu. , Petr Fiala, kujiuzulu.
Maandamano hayo ulikuwa mkusanyiko yalikuwa ya pili , kushinikiza kutokomezwa kwa umaskini.
Waandamanaji, wazungumzaji pamoja na kiongozi wa chama hicho cha uanaharakati Jindrich Rajchi waliilaumu EU na serikali ya Czech kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu, wakiitaka serikali iliyoundwa na muungano wa vyama vitano kujiuzulu. Chama cha Rajchi hata hivyo hakina kiti hata kimoja bungeni, lakini amedai kuwa chama hicho kiko tayari kuendeleza maandamano hayo .
Waandalizi wameapa kuandaa mikutano zaidi, huku nyingine ikipangwa kufanyika tarehe 28 Septemba, siku ya jimbo la Czech, isipokuwa kama serikali itajiuzulu kufikia tarehe 25 Septemba.
Fiala, kiongozi wa chama cha Civic Democratic (ODS) na profesa wa zamani wa siasa, alipuuzilia mbali maandamano hayo akisema ni ya itikadi kali na yaliyochochewa na propaganda za Urusi.
Hata hivyo, sauti zisizo za upinzani zimeonya dhidi ya matokeo mabaya yanayoweza kusababishwa na mzozo wa nishati wa msimu wa baridi unaokuja, ambao Fiala anatazamiwa kujadiliana na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz atakapozuru Prague siku ya Jumatatu.