Idadi ya watu wanaokimbia machafuko katika jimbo la Darfur huko Sudan inaripotiwa kuongezeka kufuatia wimbi jipya la mauaji ya kikabila.
Taarifa zaidi zinasema, kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaotoroka ghasia mpya katika eneo la Darfur nchini Sudan, shirika la usaidizi la matibabu linasema.
Mashuhuda wameshutumu vikosi vya Rapid Support Forces washirika wake kwa kutekeleza mauaji ya kikabila dhidi ya watu wasio Waarabu huko Darfur Magharibi.
RSF haikutoa maoni yake mara moja kuhusu madai hayo lakini awali ilisema haikuhusika katika kile ilichokitaja kuwa “mgogoro wa kikabila”.
Watu wanaokimbilia Chad kutoka Sudan, wameelezea juu ya ongezeko jipya la mauaji ya kikabila katika jimbo la Darfur Magharibi, wanamgambo wa RSF walipoiteka kambi kuu ya jeshi katika mji mkuu wa jimbo hilo, El Geneina.
Wanamgambo wa RSF wamekuwa wakipambana na jeshi rasmi tangu Aprili mwaka huu katika mzozo ambao umewalazimisha wakaazi wengi wa Darfur kuyahama makazi yao.