Mashirika ya misaada ya kiutu na ya haki za Binadamu yamesema maelfu ya Watu Manusura wa shambulizi la kigaidi kwenye Mji wa Palma, Jimboni Cabo Delgado Msumbiji wameokolewa jana.
Jumatano iliyopita Wanamgambo wenye itikadi kali walianza kufanya mashambulizi katika mji huo wenye hazina ya gesi na kulazimisha Watu 200 wakiwemo wa Wafanyakazi wa kigeni wa kampuni ya gesi kukimbilia kwenye Hoteli na kukaa zaidi ya siku tatu kabla ya kuokolewa.
Tangu Oktoba 2017 Wapiganaji wenye itikadi kali wamevizingira Vijiji na Miji katika maeneo mbalimbali ya Kaskazini mwa Msumbiji na kusababisha karibu Watu 700,000 kuyakimbia makazi yao.
ULIPITWA? TAZAMA HAPA LIVE RAIS SAMIA SULUHU AKITANGAZA KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA BANDARI NA MENGINE.