Maelfu ya Waniger walikusanyika karibu na kambi ya kijeshi ya Ufaransa huko Niamey kusherehekea kuondoka kwa balozi wa Paris mapema wiki hii, takriban mwezi mmoja baada ya utawala wa kijeshi kumwamuru aondoke.
Lakini wanaharakati wanaoipinga Ufaransa wanasema vita bado haijaisha.
“Ushindi huu sio, ukipenda, ushindi kamili wa mapinduzi haya, ni mwanzo tu. Tunatoa wito kwa wakazi wote wa Niger kukusanyika kama mmoja hadi mwanajeshi wa mwisho wa Ufaransa aondoke Niger, alisema muandamanaji Mohamed Abdou-Latif.
Mwanaharakati mwingine, Ibrahim Boubacar, alikubali.
“Tumefurahi sana. Lakini kwa sababu balozi amekwenda haimaanishi kwamba tutabaki nyumbani na kusema ‘Imekwisha, tumeshinda’ hapana, tutaendelea na mapambano,” sema.
Sasa wanasubiri Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake wapatao 1,500 kutoka Niger, jambo ambalo Paris inasema litafanyika kabla ya mwisho wa mwaka, jambo ambalo litakuwa pigo kwa ushawishi wake nchini humo.
“Tumeridhishwa zaidi au kidogo na ratiba ya kujiondoa,” alisema mandamanaji mwenzake, Issaka Tondi Tassiou.
“Kujua kidogo juu ya vifaa, ni vifaa ambavyo vimetumika kwa miaka 12, usakinishaji na kadhalika. Kwa hiyo, kukibomoa, kukifunga, na kukiondoa huchukua muda.”
Ufaransa imewaweka wanajeshi nchini Niger kama sehemu ya kikosi cha kupambana na jihadi katika eneo hilo.
Wakati huo huo, utawala mpya unasema unapanga uhusiano wake wa siku za usoni na Paris, ambao aina yake itaamriwa na watu wa Niger.