Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Deogratius Ndejembi amesema maendeleo ya teknolojia pamoja na ukuaji wa digitali nchini umesaidia kupunguza migogoro ya ardhi kutokana na wizara ya ardhi kuja na mifumo ambayo imewezesha utatuzi wa malalamiko katika sekta ya ardhi.
Waziri Ndejembi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa bidhaa ya kidigitali ya HUAWEI KIT ambapo amesema maendeleo ya kidigitali nchini yamepelekea serikali kuunganisha mifumo ambayo kwa wizara ya ardhi kupitia mfumo wa E ardhi umesaidia kuongeza kasi ya utoaji hati kwa njia ya kiektroniki pamoja na wananchi kutambua mipaka ya viwanja vyao na hivyo kuepusha utapeli katika sekta ya ardhi.
Aidha Ndejembi amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya kidigitali kwa kuwekeza katika ujenzi wa minara ya mawasiliano pa moja na kuwekeza katika mifumo ya kidigitali ili kurahisisha utoaji wa huduma.