Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF kuendelea kusimamia ujenzi wa Minara mbalimbali ya mawasiliano nchini na kuhakikisha vijiji vyote ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya mitandao viunganishwe ili kupata huduma ya mawasiliano.
Dkt. Mpango ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Ofisi za makao makuu ya mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF hii leo jijini Dodoma ambapo asema kuwa ——— “wananchi wetu wana haki ya kupata mawasiliano ya uhakika wakati wote ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kichumi husasani kipindi hiki ambapo huduma nyingi zinawezeshwa na mawasiliano, kwani bado kuna sehemu wananchi hawawezi kupata huduma ya mawasiliano”
“Wizara ishirikiane na wadau wengine katika kupata fedha zitakazowezesha UCSAF kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo yasiyo na huduma ya televisheni na redio nchini”
Aidha Makamo wa Rais Mpango ameielekeza UCSAF kuoboresha kasi ya Internet katika matumizi ya kimtandao kutoka maeneo yaliyo na 2G kufikia 4G na 5G ili kuendana na kasi iliyopo kwa sasa ulimwenguni.