Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja habari zilizoandikwa ni hii ripoti kwenye gazeti la Jambo Leo yenye kichwa cha habari ‘Ripoti 61% wahitimu elimu ya juu ni vilaza’
#JamboLEO 61% ya wahitimu vyuo vya elimu ya juu Tanzania, hawana sifa za kushindana ktk soko la ajira pic.twitter.com/Jktazyhnrm
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
Gazeti la Jambo Leo katika ukurasa wake wa mbele limeripoti ripoti kuhusu mtazamo wa waajjiri katika nchi za Afrika Mashariki iliyochapishwa mwaka juzi, katika ripoti hiyo imeonesha kuwa asilimia 61 ya wahitimu katika vyuo vya elimu ya juu Tanzania, hawana sifa za kushindana katika soko la ajira.
Hali hiyo kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyojumuishwa katika taarifa kuhusu usawa katika jamii ya Afrika Mashariki iliyotoka mwishoni mwa wiki iliyopita, imetilia shaka uwekezaji wa elimu ya juu, kwamba huenda uwekezaji wa pata potea.
Katika ripoti hiyo ya mtazamo wa waajiri iliyochapishwa mwaka juzi na Taasisi ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) kwa kushirikiana na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), imeeleza kuwa katika tatizo hilo katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania ni ya pili kwa kuwa na wahitimu hao wasio na sifa.
Nchi ya kwanza kwa mujibu wa ripoti hiyo kwa kuwa na wahitimu wa aina hiyo ni Uganda, ambayo imetajwa kuwa na asilimia 63 ya wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, wasio na mbinu kuhusu soko la ajira.
Burundi imetajwa kuwa ya tatu baada ya Tanzania ambayo ina asilimia 55; Rwanda ya nne kwa kuwa na asilimia 52 na Kenya ikiwa na wahitimu wachache wa aina hiyo ambao hata hivyo ni asilimia 51 ya wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu
#MWANANCHI Mahakama kuu yampunguzia mamlaka DPP ya kuwanyima dhamana watuhumiwa kwa sababu yanakiuka katiba pic.twitter.com/IqwwJsvY3H
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#MWANANCHI Watumishi Sengerema wasaini mara tatu kuanzia usiku wa manane kwenye mkesha wa mwenge pic.twitter.com/HLTf6cZcQv
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#MWANANCHI Kada wa CCM Hai, Mbuki Ratwei Mollel auawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye bodaboda pic.twitter.com/wZfL1NxtI1
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#MWANANCHI Mbowe, Lissu waitwa kujieleza kwenye sekretarieti ya maadili ya viongozi kuhusu matamshi waliyoyatoa pic.twitter.com/WLTTGAtaNG
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#NIPASHE Majina ya wanafunzi wasio na sifa vyuo vikuu kutangazwa mwezi ujao na kuondolewa masomoni pic.twitter.com/9Zwx0T4Hav
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#NIPASHE Kadi ya kumtambulisha mwenye betri yaagizwa Afrika Kusini kumuwezesha kutofanyiwa ukaguzi wa kielektroniki pic.twitter.com/WLw6zyw8Uh
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#NIPASHE Wataalamu wa mambo ya kijamii wamesema kuhamia Dodoma kunaweza kuvuruga familia za watumishi wa umma pic.twitter.com/jjhxQQxB45
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#NIPASHE Mme alalamikiwa kumfukuza mke, Wilayani Bahi, Dom kutokana na madai ya kubakwa na shemeji yake na kumshtaki pic.twitter.com/wmZngbEA6A
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#MTANZANIA Lema amtumia waraka mzito Rais Magufuli, amtaka atafakari uzuiaji mikutano ya kisiasa pic.twitter.com/6IpUcqAAv7
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#MTANZANIA Songwe imetajwa kuwa na changamoto ya upitishaji kinyemela wa dawa za kulevya kupitia mpakani mwa Tunduma pic.twitter.com/UxTuTAhjqS
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#JamboLEO Serikali kupiga marufuku wanaokwenda kuona wagonjwa wakiwa na simu, lengo ni kuzuia kupiga picha wagonjwa pic.twitter.com/V0TtITxlS0
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#JamboLEO Serikali kufuta sheria ya magazeti ya mwaka 1976 inayompa mamlaka waziri kufuta au kufungia gazeti pic.twitter.com/5Ao4Aq8pxV
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
#HabariLEO Imeelezwa maambukizi ya ugonjwa wa ini ni makubwa mara 10 zaidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI pic.twitter.com/eo6iXQE8QF
— millardayo (@millardayo) August 9, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI AUGUST 09 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI