Halmashauri ya Wilaya Kigamboni jijini Dar es Salaam imewataka Mafundi ujenzi kuwa na utamaduni wa kuunganisha umoja wao ili Kutoa fursa kwao kuweza kutatua Changamoto zinazo wakabili kwenye Shughuli zao na hatimaye kupatiwa utatuzi kupitia Ofisi ya wilaya.
Akiwa kwenye mafunzo ya kutumia Tekonolojia ya kisasa katika Ujenzi kwa mafundi yaliyo andaliwa na Kampuni ya Magic Builders Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt Faustine Ndungulile ametumia Jukwaa hilo kuwataka mafundi kuwa na Jumuiya moja itakayo waunganisha kikazi katika shughuli za kiuchumi.
Akielezea dhamira ya mafunzo hayo ISMAIL MWANGA ambaye ni Meneja masoko wa kampuni ya Magic builders amesema Kampuni hiyo imekua na utamaduni wa kutoa kwa jamii sehemu ya kile wanachokipata ikiwemo kuelimisha mafundi wa ujenzi nchini.