Mratibu wa Mafunzo, Dkt. Rizati Mmary ambaye ni Mchunguzi Lugha Mkuu- BAKITA, amesema wataendelea na mafunzo ya kiswahili sanifu kwa Waandishi Waendesha Ofisi (Masekretari) ambayo yataanza tena Oktoba 07 hadi 12, kisha Oktoba 14-19, Oktoba 21-26 na 28 Oktoba-02 Novemba 2024.
Lengo la kuongeza muda huo ni kuwapa nafasi Waandishi Waendesha Ofisi wote kushiriki katika mafunzo hayo, kwa kutambua umuhimu wao katika ofisi mbalimbali
Dkt. Rizati amewashukuru Waandishi Waendesha Ofisi na Waandishi wa taarifa rasmi za Bunge kwa ushirikiano wao wakati wote wa mafunzo.
Amewaomba wote waliopata mafunzo hayo wakawe mabalozi wazuri katika ofisi zao na hata nje ya ofisi.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kumalizika kwa mafunzo Kwa Waandishi waendesha ofisi zaidi ya 500 yaliyofanyika Morogoro yenye lengo la kufundisha matumizi ya kiswahili sanifu na fasaha kwenye uandishi.
Amesema mpango wa Serikali ni kuipeleka lugha ya kiswahili kimataifa hivyo wameanza kutoa mafunzo kwenye kila kundi ili kuacha kutumia maneno ya yasiyofaa katika jamii hasa Vijana ambao wanatumia maneno ya mtaani ambayo hayapo kwenye kamusi.