Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema bei za mafuta ya kupikia zimepanda kwa kuwa 55% ya mafuta ya kupikia yanayotumiwa nchini yanaagizwa kutoka nje hasa Malaysia.
Amesema Malaysia hutumia vibarua kuvuna chikichi, kutokana na #COVID19 vibarua wamekosa uhuru wa kwenda Malaysia na kufanya uzalishaji kuwa mdogo na bei kupanda.
Sababu nyingine ni kupanda kwa bei ya soya ambayo pia hutumika kuzalisha mafuta ya kupikia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji duniani.