Taarifa iliyotolewa leo July 18 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Sylvester Michael Mpanduji kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO).
Uteuzi wa Prof. Sylvester Michael Mpanduji umeanzia leo July 18, 2016, kabla ya uteuzi huu Prof. Sylvester Michael Mpanduji alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). Prof. Sylvester Michael Mpanduji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Omary Jumanne Bakari ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt.Winnie Mpanju-Shumbusho kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa – Dodoma. Kabla ya Uteuzi huo, Dkt. Winnie Mpanju-Shumbusho alikuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) lenye makao yake makuu Mjini Geneva nchini Uswisi na alimaliza mkataba wake tangu December 2015.
Uteuzi wa Dkt. Winnie Mpanju-Shumbusho umeanza July 18 2016. Dkt. Winnie Mpanju-Shumbusho anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Donan William Mmbando ambaye ameomba kupumzika kutokana na sababu binafsi.
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI AELEZA AMBAVYO ALILALA USIKU WA MANANE ILI KUPATA WAKURUGENZI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI