Shirika la Viwango nchini (TBS) limesema kuwa magari yote kutoka nje yanayokuja nchini ndani ya makasha ‘Container Motor Vehicles’ kuanzia sasa hayatakaguliwa tena bandarini bali yataruhusiwa kutoka nje kwa masharti maalum.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa shirika hilo, Roida Andusalime imebainisha kuwa utaratibu huo umewekwa kwa magari hayo kukaguliwa nje ya bandari katika kituo cha UDA kabla ya kusajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Kwa magari yanayokwenda katika maghala ya forodha kufanyiwa ukaguzi na kubainika kuwa na hitilafu yataruhusiwa kwenda kwenye maghala hayo kwa masharti kwamba baada ya kulipiwa ushuru yatatengenezwa na kukaguliwa tena kabla ya kusajiliwa na TRA” Roida
MAPYA GENIUS WA HESABU APATA SHULE YA KISHUA “KURUSHWA DARASA NI KIBOKO, ANAWAZIDI DARASA LA SABA”