Nimekurekodia Magazeti yakisomwa hewani kwenye Redio leo February 20, kwenye show ya Power Breakfast ya Clouds FM, yakisomwa na kuchambuliwa na .
Baadhi ya taarifa zilizochukua uzito kwenye Magazeti ya leo ni pamoja na ile inayosema aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu amesema atagombea Ubunge, Lori la mafuta laanguka huko Mbeya na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa wakati wakijaribu kuiba mafuta, Askari wapunguzwa katika zoezi la kukabiliana na wahalifu Tanga, baadhi ya maduka Dar yaendelea kuuza dawa zilizofutiwa usajili, wizi wa mtandao bado unaendelea kuliza mabenki duniani, watu wenye ulemavu wa ngozi wamepanga kufanya maandamano kwenda Ikulu, Umoja wa Mataifa umeingilia kati mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kulaani vikali matukio hayo, uandikishwaji wa wapiga kura kwa kutumia mfumo wa BVR watiliwa shaka, Serikali imeshauriwa kutoongeza ushuru kwenye vinywaji vikali ili kuwezesha viwanda kukua na kutumia malighafi za ndani na Chama cha ZANUPF kimepanga kutumia dola milioni moja kwa ajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe anaetimiza miaka 91.
104.1 Clouds FM inasikika ukiwa Bukoba.
Bonyeza play hapa chini ili kusikiliza stori zote…
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook