Hizi ni baadhi ya zilizopewa headlines kwenye Magazeti ya leo MAY 22 2015.. Utazipata zote pia kwenye sauti ambayo nimeirekodi na kukuwekea hapa.
Baada ya mgomo wa wanafunzi Chuo cha Dar es Salaam sasa mgomo umehamia Chuo Kikuu Dodoma, wamesema hawatoingia darasani mpaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifika chuoni hapo, stori nyingine inahusu NEC kusema kwamba kutakuwa na utaratibu wa kila aliyejiandikisha kupiga kura hata kama atakuwa amehama sehemu alipojiandikishia.
Mgomo wa wafanyabiashara walemavu Dar nao uko kwenye vichwa vya habari, wafunga barabara Dar kwa zaidi ya saa tano.. kingine ni baadhi ya ndugu na jamaa ambao ndugu zao walifariki kwenye ajali ya MV Bukoba wamelalamikia Serikali kutojali siku ya kumbukumbu ya ajali hiyo, kuna stori pia ya wanafunzi 44 wa Ngorongoro wametimuliwa kutoka shule za Kenya, kisa kinachohusishwa ni ishu ya kufukuzwa kwa wahamiaji haramu Loliondo.
Mbunge wa Rombo Joseph Selasini amezungumzia kuumizwa na stori wa wanawake kuagiza wanaume toka Kenya, utamsikiliza pamoja na uchamnbuzi wote kwenye sauti hii hapa.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.