Magazeti ya Agosti 4 2015 yako mtaani na vichwa vyake vikubwa vya habari, nimefanya jitihada ya kukusogezea zile zote kubwakubwa zilizoweka vichwa vya habari magazetini leo…
Kuna stori kubwa zenye headlines zake mtaani leo, iko inayohusu Prof. Ibrahim Lipumba kuachia ngazi na mgogoro mzito unaotikisa, chanzo Lowassa?.. Zanzibar imesema haitotambua umoja wa UKAWA na maamuzi ya kutambua umoja huo ni ya Tanzania Bara na sio yao… Dk. John Magufuli kuliteka jiji kwa kuchukua fomu ya Urais leo ataongozana na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan kwenye ofisi za NEC.
CHADEMA yamuweka pembeni Dk. Wilbroad Slaa, wameamua kumpumzisha kwa muda baada ya kutoafikiana na maamuzi ya Chama kumkaribisha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
ADC yaanza mchakato wa kumpata mgombea Urais wa mwaka 2015, leo ikiwa ni siku ya mwisho ya watu kujiandikisha idadi wapiga kura Mil 2.6 waandikishwa kupiga kura na BVR Dar, hii ni aslimia 94%.
Rushwa yamtia kichefuchefu Rais Jakaya Kikwete, Mzee Peter Kisumo afariki dunia jana saa moja usiku kwenye Hospitali ya Muhimbili, kifo chake kimesababishwa na maradhi ya figo.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti @CloudsFM nimekurekodia na kukuwekea hapa chini.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos