Jumanne ya October 6 2015 imeanza na uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM, jukumu langu kwako siku zote ni kuhakikisha zile zote kubwa kubwa za siku hazikupiti… kama hukuzisikia zote basi karibu ucheki na hizi nyingine kufidia.
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila kuagwa kesho jijini Dar es salaam na kisha kusafirishwa kwenda kijijini kwao Milo mkoani Njombe, kwa sasa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi, Lugalo.
Chama cha ACT Wazalendo kimefuta mikutano yote ya Dk. Willbroad Slaa kwa hofu ya usalama juu ya maisha yake, Dk. Slaa alishakubali kupanda kwenye majukwa ya ACT Wazalemdo ili kupambana na vita dhidi ya Ufisadi baada ya chama chake cha zamani kutelekeza vita hiyo.
TAKUKURU kulipua watu wala rushwa baada ya Uchaguzi Mkuu October 25, mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa alimshauri Namelok Sokoine kuachana na CCM Monduli lakini amekataa ushauri wake na sasa Lowassa amesema hana urafiki na mtu yoyote wa CCM.
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Magufuli jana alihutubia Karatu na kumwagia sifa Dk Willboard Slaa aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo na kusema kuwa ni kiongozi mzuri wa upinzani, muadilifu asiependa ufisadi huku akiwaahidi watu wa Karatu elimu ya bure, kusaidia Sekta ya Utalii pamoja na kuhakikisha anatatua matatizo yao.
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi amesema Idadi ya Watanzania waliofariki Mecca yafika 8 huku wengine 35 hawajulikani walipo… Polisi juzi walilazimika kufyatua risasi hewani kwenye kituo cha Polisi cha Himo ili kusambaratisha fujo za vijana waliotofautiana kimtazamo kwenye kikao cha kura za maoni.
Wakatoliki wameruhusiwa kusali jumamosi siku ya October 24 ili kuwapa nafasi waumini wengi kupata fursa ya kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu siku ya jumapili October 25… kundi la nyani wasumbufu kwenye kijiji kimoja cha Zimbabwe limevamia kituo cha Radio cha Ya.FM kwa kula nyaya za umeme kitendo kilichosababisha matangazo ya asubuhi ya radio hiyo kupotea ghafla hewani.
Tunaomba radhi kutokana na tatizo la sauti.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE