Kutoka kwenye Magazeti ya Jumanne 11 August 2015 hapa nina Uchambuzi wa Stori kubwakubwa za leo mtu wangu.
Dk. John Magufuli asema ushindi wa CCM upo palepale, waliohama wamekiacha Chama salama na mwaka huu watafanya kampeni za kisayansi, Mwigulu Nchemba amesema ni rahisi sana kumnadi John Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.
Edward Lowassa alisimamisha Jiji kwa saa kumi kwenye safari ya kuelekea ofisi za NEC kuchukua fomu za kugombea Urais, shughuli za Mahakama zasimama pia, waendesha pikipiki wamsindikiza kwa mbwembwe na manjonjo.
Kundi la vibaka latikisa UKAWA, wafanya vurugu kwenye msafara wa Edward Lowassa, wavamia maduka, wapora mali za wafanyabiashara na wapita njia… Tafrani yazuka Ofisi za NEC baada ya Waandishi wa Habari kuzuiwa kuingia ndani ya chumba cha kuchukulia fomu ya Urais.
Dr. Mohammed Bilal akanusha uvumi wa kukihama Chama cha CCM... TCRA imetangaza kiama kwa watumiaji vibaya na wahalifu wote wa mitandao, watangaza Sheria ya Uhalifu ya Mitandao kuanza kutumika rasmi September 01 2015.
Stori nyingine kubwa kwenye Magazeti inahusu Kanisa moja kuwazuia zaidi ya waumini 4,000 kujiandikisha kwenye BVR… Unaweza kuzisikiliza stori zote kutoka #PowerBreakfast @CloudsFM.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos