Ni tarehe 13 October 2015 na uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umesikika moja kwa moja kutoka 88.5 Dar es salaam. Inawezekana hukuzisikia zote kwenye kuperuzi na kudadis na kama zilikupita basi karibu ucheki na hizi nyingine.
Lowassa awataka Mwanza kujiandaa, Wapiga kura halali ni milion 22 huku watu milion 1 wabainika kuwa feki , Dk. Magufuli asema hataki mchezo, Membe amvaa Lowassa, Dk. Slaa amwagia sifa Zitto Kabwe, UKAWA yajiandaa kushinda Urais, NEC yavionya vyama vya Siasa.
Rais Jakaya Kikwete kuzindua mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi maeneo ya Kinyerezi itakayo kuwa suluhisho la tatizo la umeme nchini, NEC yatangaza idadi mpya ya wapiga kura kuwa milion 22.75 huku majina ya watu milioni 1 yabainika kuwa feki, asilimia kubwa wakiwa wahamiaji waliojiandikisha zaidi ya mara moja.
TWAWEZA kuandaa mdahalo wa wagombea Urais kwa ajili ya kuwapa wagombea nafasi ya kujibu maswali tofauti kutoka kwa wananchi, mdahalo huo umepangwa kufanyika tarehe 18 October… Rais mstaafu Benjmin Mkapa anaendelea kuruka na choppa kwa ajili ya kumnandi mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli, asema kitendo cha mgombea Urais wa CHADEMA Edward Lowassa kutaka kuondoa umasikini ndani ya siku 100 ni kauli ya kuwadanganya vijana.
Vuguvugu la kisiasa na uchaguzi mwaka huu wa 2015 halipo kwetu tu bali hata nchi nyingine za kiafrika baadhi zikiwa; Ivory Coast na Guenea, Mgombea Urais wa CHADEMA Edward Lowassa asema hesabu zao za Uchaguzi wa October 25 zimekubali na hivyo watashinda Uchaguzi Mkuu October 25 na kuwaacha CCM kwa mbali na Dk. John Magufuli ameahidi kutokufanya mchezo na mafisadi wa nchi wanaotumia rasilimali za nchi ovyo huku maskini wakiendelea kuumia.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast kwenye hii sauti hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.