Ni Jumanne 20 October 2015 na kama kawaida lazima asubuhi ianze na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM. Ninazo zote kubwa za leo kwenye kuperuzi na kudadis, kama zilikupita unaweza ukacheki na hizi nyingine kufidia.
Rais Jakaya Kikwete ameiaga Ikulu na watumishi wake, asema miaka 10 ya uongozi unatosha kukamilisha agenda yake ya msingi na haitaji miaka mingi zaidi kukamilisha agenda nyingine kwani Rais ajae atampokea kijiti na kuendelea pale alipoishia, amewataka watumishi wa Ikulu kumuonyehsa Rais ajae ushirikiano mkubwa na wakutosha kukamilisha agenda nyingine za maendeleo ya nchi.
Viongozi wa dini wasihi amani juu ya Uchaguzi Mkuu October 25, wamewaomba Watanzania kupinga dalili zote zinazoashiria vurugu ya amani pia wamewataka viongozi wa Serikali pamoja na NEC kuhakikisha hatua zote za ulinzi wa amani zinachukuliwa ili kuepusha vurugu zozote zile zinazoweza kutokea.
Mgombea Urais CCM Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein asema kuwa akipata nafasi ya kuwa Rais ataigeuza Zanzibar kuwa kama miji mikubwa ya dunia kama Dubai kwa miradi mbalimbali, Mgombea Urais CCM Tanzania bara, Dk. John Magufuli amewataka Watanzania kukiamini chama cha CCM kwani kimejengwa kwenye misingi ya amani na ahadi zote anzozitoa atahakikisha anazitekeleza kikamilifu ndani ya uongozi wake… mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa ameahidi kutokomeza tatizo la foleni Tunduma ndani ya siku 20 ikiwa akipata ridhaa ya kuongoza nchi kwa awanu ya tano.
Kesi ya mita 200 kuanza leo, jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam leo kuanza kusikiliza kesi ya Kikatiba kuhusu Sheria ya haki ya mpiga kura kukaa umbali wa mita 200 kama ni sahihi au sio sahihi… Rais Jakaya Kikwete amemteua Dk. Katarina Revocatti kuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na John Kayoza kuwa msajili wa Mahakama ya Rufani.
Unaweza pia ukasikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE