Kama kawaida Jumatatu ya kila wiki huanza na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM, pengine ulikuwa mbali na radio yako na habari za magazeti zimekupita, ninazo hapa chini baadhi ya stori zilizosikika leo.
Watalaamu wa masuala ya uhamiaji wamesema dunia inatakiwa kuangalia upya suala la mgogoro wa uhamiaji na mipaka, Mgombea Urais kupitia CCM John Magufuli asema akichaguliwa kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya tano ataiendesha nchi kwa utaratibu na sio kidikteta kama wengi wanavyodai.
Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa asema yeye ndiye anaetosha kuondoa umasikini Tanzania, CUF Zanzibar imetangaza ilani ya Uchaguzi, Mgombea Urais Zanzibar kupitia CUF Maalim Seif asema kama Zanzibar ikimpatia ridhaa ya kuwa Rais wao atapambana na vitendo dhidi ya madawa ya kulevya.
Awamu ya kwanza ya Mabasi 138 ya DART yawasili nchini kutoka China, hukumu ya Emmanuel Mbasha kutolewa leo Mahakama ya Wilaya ya Ilala na hofu kubwa yatanda Arusha baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa ni Volcano kulipuka Mlima Meru na kusababisha vumbi zito kutanda angani na kufunika mlima huo.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast nimeiweka hapa chini, bonyeza play kusikiliza.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos