Good Morning mtu wangu, uchambuzi wa magazeti @CloudsFm umekupita? kazi yangu ni kuhakikisha zile zote kubwa kwenye kuperuzi na kudadis hazikupiti, lakini kama ilikupita na hukuisikia basi karibu ucheki na hizi nyingine.
Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Magufuli kutikisha jiji la Dar es salaam kwa siku tatu, Umoja wa Africa Mashariki, EAC yaisifu Tanzania kwa kudumisha demokrasia kwa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano na kubadilisha viongozi wa nchi ngazi ya juu kila baada ya miaka kumi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameviomba vyama vya kisiasa kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu October 25 huku akiwasihi watambue kuwa kuna kushinda au kushindwa, awaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Rais Jakaya Kikwete amelitaka jeshi la polisi nchini kuwa waangalifu juu ya watu watakaoleta fujo na vurugu siku ya Uchaguzi Mkuu… Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa jana aliongoza mamia ya wananchi kwenye mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha NLD Dk. Emmanuel Makaidi.
Mgombea Urais kupitia chama CCM Dk. John Magufuli amesema Tanzania inaweza kuwa kama nchi za Ulaya ikiwa tu akipewa ridhaa ya kuongoza nchi kwa awamu ya tano, amesisitiza kwenye ahadi zake kufufua viwanda na pia kuanzisha viwanda vingine.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha na wenzake sita leo kufikishwa Mahakamani mjini Mpanda mkoa wa Katavi kwa mashtaka mawili ikiwa kosa la kufanya mkutano na kuingia kwenye kambi ya wakimbizi bila kibali.
NEC imetoa ufafanuzi kuhusu namna ya kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu October 25 na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam leo kusikiliza kesi ya haki ya mpiga kura kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura.
Unaweza pia kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini kwenye hii sauti.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.