Uchambuzi wa magazeti leo 25 September 2015 umesikika moja kwa moja kutoka @CloudsFM ‘The Peoples Station’, na kama kawaida ripota wako wa nguvu anazo zile zote kubwa za leo kwenye kurasa za magazeti.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Celina Kombani afariki dunia jana nchini India alipokuwa anapata matibabu, Mahujaji 117 wapoteza maisha Mecca, matokeo ya utafiti ya TWAWEZA yaendelea kupingwa huku UKAWA wasema utafiti huo umelenga kuibeba CCM, James Mbatia ametoa mwaliko kwa TWAWEZA katika mdahalo huru ili kujibu maswali yaliokosa majibu kuhusu utafiti huo.
Kampuni ya IPSOS imekana ripoti iliyosambaa jana ikielezea matokeo yake ya utafiti wa hali ya kisiasa nchini huku utafiti huo ulionyesha kuwa kama Uchaguzi mkuu ungefanyika mwezi September Mgombea Urais CCM John Magufuli angeshinda kwa 62% na Mgombea Urais CHADEMA Edward Lowassa angeshinda kwa 31% na Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo Anna Mgwila angeshinda kwa 0.3%.
Mgombea Urais CHADEMA Edward Lowassa asema hatakubali kushindwa mpaka pale itakapobainika kuwa Uchaguzi Mkuu ulifanyika kwa haki na taratibu zote zilifuatwa bila wizi wa kura, Rais Jakaya Kikwete amesema hamshangai mgombea Urais kupitia Chama chake Dk. John Magufuli kukosoa utendaji kazi wa Serikali yake katika kampeni zake, asema yuko sawa kwani kila kiongozi ana namna yake ya kuongoza.
Waangalizi wa Umoja wa Ulaya EU wanaendelea kuwasili nchini, Maafisa polisi nchini South Africa wanamshikilia mwanaume mmoja kutoka Ujerumani aliyekamatwa kwa madai ya kuhifadhi sehemu vya sehemu za siri 21 za wanawake kwenye jokofu, upelelezi juu yake bado unaendelea.
Nimekuwekea sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE