Good Morning mtu wangu, leo ni tarehe 26 October 2015 na kama kawaida lazima asubuhi ianze na uchambuzi wa stori zote magazetini @CloudsFM. Kazi yangu ni kuhakikisha kubwa zote za leo hazikupiti, ninazo hapa zote za leo kwenye kuperuzi na kudadis.
Matokeo ya Urais kutangazwa siku ya Alhamisi, CCM, CHADEMA watoa kauli, mamilioni wajitokeza kupiga kura, karatasi za kura zaokotwa shule ya sekondari, Dk. Shein asema upinzani wawe tayari kukubali matokeo.
NEC imesema kwanzia leo saa tatu asubuhi itaanza kutoa matokeo ya Uchaguzi katika ngazi za Ubunge mpaka saa kumi jioni na ifikapo tarehe 29 October watatangaza matokeo ya Urais wa Uchaguzi mkuu… Uchaguzi Dar shwari huku wananchi wengi wakijitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura na kuchagua viongozi.
Wagombea Urais jana walikuwa miongoni ya mamilioni waliojitokeza kupiga kura siku ya tarehe 25 October 2015, Dk John Magufuli na Edward Lowassa wote walijitokeza kupiga kura kwenye vituo vyao huku kila mmoja akijinadi kuwa mshindi. Dk John Magufuli aliwataka wananchi wamtangulize Mungu kwani yeye ndio muweza wa yote, huku Edward Lowassa asema atashinda uchaguzi mkuu kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki na kama hakutotokea wizi wa kura.
NEC imesema itapanga namna ya wananchi wa Sumbawanga na wilaya ya Kindondoni kupiga kura na wale wote waliojihusisha na vitendo vya kuchochea fujo watachukuliwa hatua kali za kisheria… Watu wenye ulemavu wa macho wadai kukosa kalamu maalumu zitakazowawezesha kupiga kura.
TCRA imepiga marufuku kwa vituo vya utangazaji kutangaza matokeo yasiyo sahihi ya Uchaguzi Mkuu bila kutangazwa na NEC kwanza… NEC imesema matokeo ya Urais yatatangazwa siku ya Alhamisi tarehe 29 October na Rais atakayetangazwa atakabidthiwa cheti chake kesho yake.
Rais Jakaya Kikwete kustaafu rasmi kama Rais wa Tanzania tarehe 5 November 2015… Baadhi ya waangalizi wa Kimataifa waeleza hali waliyoiona siku ya Uchaguzi Mkuu October 25 na kudai kuridhishwa na mchakato mzima ikiwa na muamko wa Watanzania kujitokeza kupiga kura licha ya matatizo madogo kujitokeza baadhi ya maeneo.
Unaweza ukasikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE