Headline iliyotawala Magazeti ya leo inahusu ufisadi mkubwa TTCL ulioibuliwa na Mbunge Habib Mnyaa, nyingine inahusu chama cha ACT- Wazalendo kuteua viongozi wa Chama chao, maofisa 70 pamoja na wapenzi wao wametembelea gereza moja China kama ilani ya kutoshiriki ufisadi, foleni ya wanaotaka kuteuliwa CCM imeongezeka, Rais JK amewaaga Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao TZ.
Kuna dalili za kutokamilika kwa uandikishwaji wapigakura kupitia BVR.. Stori nyingine ni ishu ya Wamiliki wa Vyombo vya Habari wamesema wameunda Kamati itakayoenda Bungeni kuzuia Sheria ya vyombo vya Habari.. kingine ni foleni ya wanaowania kuteuliwa CCM imeongezeka.
Spika Anne Makinda amesema bangi iliyokuwa inaota Njombe haikuwa kali kwa sababu ya baridi.. stori zote ziko kwenye hii sauti hapa kutoka #PowerBreakfast @CloudsFM
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.